Mkimbizi by Hussein Tuwa

TSh 21,000

#B1047

Maelezo

Condition: Brand New Book Type: Paper Back Book Details Naitwa Tigga Mumba. Marafiki zangu walizoea kuniita Tigga-Mu. Lakini sasa sina marafiki tena. Mimi ni mtafiti wa mambo ya kale lakini nadhani niseme kuwa nilikuwa mtafiti wa mambo ya kale Archaelogist. Nilikuwa nina matarajio makubwa sana maishani. Nikiwa na shahada yangu ya kwanza ya utafiti wa mambo ya kale kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kazi nzuri na ninayoipenda, marafiki wachache lakini wazuri na wacheshi, jamii yangu ndogo iliyojaa upendo, na mchumba mtanashati niliyekuwa natarajia kufunga naye ndoa itakayojaa upendo, nikiwa na ndoto ya kuzaa naye watoto wawili: wa kwanza wa kike na wa pili wa kiume sikuwa na sababu ya kukosa matarajio makubwa maishani. Lakini vyote hivi vilikuja kutoweka ghafla katika tukio moja tu la kutisha na kuogopesha sana lililotokea katikati ya msitu mnene ulioko katikati ya nchi hii siku moja nilikuwa msichana mmoja mcheshi wa miaka ishirini na saba, mwenye urembo wa kuridhisha na ndoto nyingi za mafanikio mbele yangu, siku iliyofuata vyote hivi viligeuka na kuwa ndoto moja mbaya na ya kutisha sana. Ila tu mambo yaliyobadilisha matarajio na maisha yangu hayakuwa ndoto bali ni kweli kabisa. Ni vigumu sana kuamini kuwa mambo yaliyonitokea na yanayoendelea kunitokea, yananitokea mimi. Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na kuniwia vigumu kuamini kuwa ninatokewa na mambo haya, bado najikuta kuwa ni mimi peke yangu ndiye ninayeamini ukweli wa matukio haya ya kutisha. Kwani kila ninapokwenda, kila ninapojaribu kuelezea ukweli wa matukio haya, hakuna hata mmoja anayeniamini na naishia kuwa mkimbizi ninayekimbia kwa woga na wasiwasi. Na kama hiyo haitoshi, kinachouma kuliko vyote ni kwamba kwa mtu niliyekuwa na marafiki, jamaa na hata mchumba wa dhati, najikuta nikilazimika kukabiliana na masahibu haya peke yangu. Yote hii ni kwa sababu ya kushuhudia tukio moja la kutisha lililotokea katikati ya msitu mnene. Tukio lililonifanya niwe mkimbizi ndani ya nchi yangu kwa sababu sasa sina mahala popote ambapo ninaweza kujihisi salama, sina mtu yeyote ambaye nitajihisi salama kuwa naye, na wala hakuna mazingira yoyote yanayoweza kunifanya nijione salama. Mahala pekee ambapo nitajihisi salama ni pale nitakapokuwa peke yangu na mtu pekee nitakayejihisi salama kuwa naye ni mimi mwenyewe! Na mpaka nitakapoipata hiyo sehemu ya peke yangu, nitabaki kuwa mkimbizi tu peke yangu, muoga, mpweke! Na hata hapa ninapoandika maelezo haya kuhusu tukio la kutisha lililobadili kabisa mwelekeo wa maisha yangu na mtazamo wangu katika maisha kwa ujumla, niko peke yangu. Nikiwa na mtu pekee ninayemuamini katika maisha yangu

au

Bidhaa Zinazofanana