Kiswahili Kidato Cha Nne - Maeda, T.S

TZS 6,000

#B5234

Description

Kitabu hiki kimeandaliwa kwa kuzingatia muhtasari mpya wa Kiswahili kidato cha nne. Kitabu hiki kimejumuisha pia maswali yatakayomwezesha mwanafunzi kujipima na kujitathmini kwa ajili ya maandalizi ya mitihani yake ya taifa. Maeda.T.S alihitimu elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndaki ya DUCE mwaka 2009 na kutunukiwa Shahada ya Elimu (B.A.Ed) ya heshima. Tangu kuhitimu kwake alijikita zaidi katika somo la Kiswahili. Maeda.T.S ni mwalimu mzoefu katika kufundisha somo la Kiswahili. Amewahi kufundisha shule ya sekondari Green Acres, Shule ya Sekondari ya wasichana ya Cornelius, Shule yn Sekondari Mbezi Beach na Shule ya Sekondari Shaaban Robert zote za Dar es Salaam. Ameshiriki katika kutunga, kurekebisha na kusahihisha mitihani ya ngazi mbalimbali kwa elimu ya sekondari Aidha, amekuwa akifundisha kozi za Kiswahili kwa wana funzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa muda mrefu na kujipatia sifa kemkem.

or

Similar Products